Pages

Ndugu: Chinja chinja wa IS akamatwe

Mauaji ya kundi la Islamic State
Dragana Haines mke wa David Haines,mamlaka zinapaswa kumsaka na kumkamata akiwa hai mtu aliyemuua mume wake kwa kumchinja baada ya kutekwa na kundi la wapiganaji wa dola ya kiislam Islamic State wakati akifanya kazi na shirika la misaada la Uingereza.Mtu aliyemchinja David Haines na wengine tayari amefahamika kuwa ni Mohamed Emwazi.
Bi.Dragana amesema tangu alipojua kuwa mmewe David amechinjwa alijipa matumaini moyoni mwake kuwa ipo siku muuaji huyo atafahamika na hatimaye kukamatwa.Lakini baada ya kupatika kwa taarifa hizi za muuaji huyo anasema kuwa itakuwa faraja ya pekee kwa familia za kila aliyeuawa kinyama na wauaji hao, kwa sababu kama atakutwa amekufa anaona hicho kitakuwa ni kifo cha heshima kwa Mohamed Emwazi, lakini maombi yake ni kwamba kukamatwa akiwa hai na afe baadaye.
Kwa upande wake Barak Barfi ambaye ni msemaji wa familia ya Sotloff iliyopoteza ndugu yao pia, anasema kuwa hawana wasiwasi juu ya kukamatwa kwake muuaji huyo Mohamed Emwazi ama JIHAD JOHN.
"Tuna Imani kubwa sana na nchi ambayo vyombo vyake vya usalama na kiintelijensia vitawakamata watu hawa.Tungependa kwenda kumuangalia muuaji huyu ana kwa ana wakati wa mashtaka yake katika mahakama ya Marekani,na pia kuona akitumikia kifungo chake, katika gereza maalumu ambako ataishi huko pekee yake katika upweke.hiyo ndiyo sheria ya Marekani na hivyo ndivyo nchi yetu inavyoshughulikia matatizo kama haya"amesema Barak.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)