Pages

Mwanza Kujembekea na Sauti Soul Feb 21 Mwaka huu

300 x 150m

Hatimaye ule mpango mzima wa kuzifungulia burudani ulioasisiwa na redio mpya ya jijini Mwanza JEMBE FM na kubatizwa jina 'JEMBEKA' unaanza rasmi jumamosi ya wiki hii tarehe 21/02/2015 ndani ya kiota cha burudani cha kitalii Jembe Beach Mwanza.

Burudani itakayo fungua mpango huo wa 'JEMBEKA' ni kutoka kwa kundi maarufu Afrika Mashariki lililovuka mipaka na sasa muziki wake kuchezwa hadi barani Ulaya kundi la Sauti Sol toka nchini Kenya ambao watapiga muziki LIVE.

Vijana wa Nyumbani JJ Band nao watakuwepo ndani ya Jembe Beach Resort kwaajili ya kumwaga burudani ya kijanja zaidi ya vile ulivyowazoea.
Kiingilio ni shilingi 10,000/= kwa tiketi za awali na Tshs 15,000/= ukinunua getini.

Tiketi zinapatikana ofisi za Jembe Fm zilizopo PPF Plaza Mwanza.
Ni chini ya udhamini wa K Vant Gin, Coca cola, ikiwezeshwa na Jembe ni Jembe, Jembe Fm, Jembe Djz na G.SENGO BLOG.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)