Pages

Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa NHIF bw Emmanuel Humba aagwa

1Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua mchango wake akiwa mwanzilishi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuwaaga viongozi na wafanyakazi wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee mwishoni mwa wiki , Mzee Emannuel Humba aliwaasa wafanyakazi wa mfuko huo kushikamana na kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha mfuko huo unafikia malengo, Katika hafla hiyo Emanuel Humba pia amezawadiwa zawadi mbalimbali. wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Michael Mhando.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE) 2Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akitoa shukurani zake kwa uongozi wa NHIF na wafanyakazi kwa ujumla kwa kuwaadalia hafla hiyo ya kuwaaga. 3Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akipokea shada la maua kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF. 4 Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katika hafla hiyo wakati akielezea wasifu wa baadhi viongozi wastaafu wa mfuko huo. 6Dr Marqus Kalinga Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa akipokea tuzo yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando 7Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akisoma wasifu wa mmoja wa wastaafu. 8Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo akikabidhi zawadi kwa mstaafu Andrew Mwilungu aliyekuwa meneja wa NHIF Pwani. 10Mstaafu Peter Daniel akitoa shukurani zake mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake katika hafla hiyo ya kuwaaga wastaafu wa Mfuko wa Bima Afya ya Taifa, kutoka kushoto wanaofurahia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando 12Baadhi ya wafanyakazi wakijadili jambo wakati wa hafla hiyo. 13Wafanyakazi wakiwa na nyuso za furaha 14 16Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando akizunguma katika hafla hiyo. 17 18Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando kushoto akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Ali Mchumo kulia na Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti 20Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Othman Rehani Mkurugenzi wa Afya ya Jamii CHF na Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey wakipitia makabrasha wakati wa hafla hiyo. 21Balozi Ali Mchumo Akisalimiana na Mkurugenzi Mstaafu wa NHIF Bw. Emannuel Humba. 22Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi Akiwasili ukumbini hapo huku akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando. 23Baadhi ya wafanyakazi wakimpokea mwenyekiti wa Bodi. 24Hapa wakiserebuka kidogo 25 26Wafanayakzi wakiwa wamejipanga huku wakifurahia jambo wakati wa mapokezi ya viongozi na wafanyakazi wastaafu wakati walipowasili kwenye ukumbi wa Diamond tayari kwa hafla hiyo 27Mzee Emanuel Humba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakiinga ukumbini hapo huku wakipokelewa na wafanyakazi. 29Baadhi ya maofisa 30 Grace Michael kushoto Hawa Katikati na Catherin wakipozi kwa picha32Wafanyakazi hao wakimpelekea keki Kaimu Mkurugenzi mkuu NHIF Bw. Michael Mhando. 33Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando pamoja na baadhi ya wafanyakazi.31Kutoka kushoto Maofisa wa NHIF Sabina Komba na Luhende Singu wakiwaongoza maofisa wenzao kufungua Shampeni wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)