Pages

Kiongozi wa upinzani auawa Urusi

Maafisa wa polisi wakiweka usalama katika eneo ambalo kiongozi wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov aliuawa
Mmoja wa wanasiasa maarufu wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Mwanasiasa huyo alipigwa risasi nne kutoka nyuma na watu waliokuwa ndani ya gari alipokuwa akitembea nje ya makao makuu ya serikali.
Bwana Nemtsov ambaye alihudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa uongozi wa rais Boris Yeltsin alikuwa akimshutumu vikali rais Vladimir Putin.
Boris Nemtsov
Alikuwa akipanga mkutano ambao ungefanyika kesho Jumapili kupinga kile alichokitaja kuwa vita vinavyoendeshwa na Urusi nchini Ukrain.
Kwenye mahojiano mapema mwezi huu bwana Nemtsov alisema kuwa alikuwa na hofu kuwa rais Putin angemuua.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)