Pages

Jifunze hapa Kuhusu Matairi ya Gari yako Pt 1

Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari yako). Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. 

Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. 

Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)