Pages

Chid Benz anusurika kwenda jela kwa kulipa faini ya 900,000 kutokana na hukumu yake ya madawa ya kulevya

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.


CHIDI BENZ HURU:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)