Pages

Askari Polisi watimua mbio huko Iringa leo mara baada ya Vurugu kati ya Wananchi na Polisi

Baadhi ya wananchi wa mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa wameizunguka moja ya gari linalodaiwa kuchomwa moto na baadhi yao kufuatia vurugu kubwa iliyotokea mapema leo.
Moto ukiendelea kuwaka barabarani.
Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6.

Wananchi wa mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo wamezua tafrani dhidi ya Askari Polisi baada ya mwanamke mmoja kupoteza maisha kwa kudaiwa kusababishwa na Askari hao waliokuwa kwenye msako wa kukamata watu wanaokunywa pombe wakati wa kazi.

Kutokana na tukio hilo, mwanamke huyo aliyepoteza Maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi awali aliamua kukimbia kwa lengo la kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la kilabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa,Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kilichopo kwenye mji huo kudaiwa kuvunjwa na kuchomwa moto kwa magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)