Pages

WAHAMIAJI HARAMU 16 WA SOMALIA WAKAMATWA NDANI YA LORI LILILOBEBA CHOKAA MKOANI MOROGORO

 Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro wakiwa wamejificha  katika  lori la mizigo lililosheni chokaa  likitokea jijini dar es salaam kuelekea mkoani mbeya Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa wananchi  ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo   Kwa upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa  vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya kujificha katika magari ya mizigo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)