Pages

VIONGOZI KUTOKA VYAMA VYA UKOMBOZI WATEMBELA IHEMI

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa IringaNdugu Jesca Msambatavangu akiwaongoza viongozi wa vyama vya ukombozi mara tu walipowasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku moja ya kutembelea chuo cha Ihemi, Viongozi hao wapo nchini kuhudhuria mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vya Ukombozi utakaofanyika tarehe 9,Septemba 2013 jijini Dar es salaam.
 Viongozi mbalimbali kutoka vyama vya ukombozi wakifurahia ngoma za asili wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa nduli tayari kwa ziara ya siku moja kukitembelea chuo cha Ihemi.
 Viongozi kutoka vyama vya Ukombozi Afrika wakionyesha ishara ya mshikamano wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwakaribisha rasmi kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kuwakaribisha viongozi wa Vyama vya Ukombozi katika chuo cha Ihemi.
 Viongozi kutoka vyama mbali mbali vya ukombozi Afrika pamoja na marafiki wa vyama hivyo kutoka China wakiangalia eneo la Chuo cha Ihemi walipotembelea leo mkoani Iringa.
 Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO Ndugu Nangolo Mbumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana kitajengwa na kusema Tanzania ni nchi ambayo imefanya kazi kubwa kulikomboa bara la Afrika.
 Sehemu ya eneo la chuo cha Ihemi mkoani Iringa ambapo kitakapojengwa chuo kikubwa cha Uongozi kwa Vijana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Katibu Mkuu wa chama cha Flerimo cha Msumbiji Ndugu Filipe Paumda pamoja na wageni wengine kutoka vyama vya ukombozi Afrika na chama rafiki cha kikomunisti cha China wakitembelea maeneo mbali mbali kwenye chuo cha Ihemi ambapo kitajengwa chuo cha Viongozi Vijana .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaonyesha viongozi kutoka vyama vya Ukombozi Afrika ,ukubwa na uzuri wa eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana Afrika kitajengwa.
 Mratibu wa Chuo cha Ihemi Ndugu Lucas Kisasa akifafanua baadhi ya mambo muhimu ya chuo hicho kwa Naibu Waziri katika Idara ya Kimataifa kutoka china Ndugu Ai Ping .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akizungmza na Billy Masetlha na Obed Bapela kutoka chama cha ANC cha Afrika Kusini wakati wa ziara yao kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa.

Viongozi mbali mbali wa vyama vya Ukombozi wakiagana na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa baada ya kukamilisha ziara yao ya siku moja ya kutembelea chuo cha Ihemi mkoani hapo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)