Pages

USIKU WA CHAKULA CHA HISANI ULIONDALIWA NA AMREF TANZANIA NA MONTAGE LIMITED WAFANA HAPO JANA SERENA HOTEL

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited Bi Teddy Mapunda akitoa shukrani kwa Wadhamini na wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani uliofanyika Jana katika Hotel Ya Serena ikiwa na Lengo na kutafuta pesa kwaajili ya Kusomesha Wakunga ili kuweza kusaidia katika kupata wakunga ambao Watatoa huduma na kupunga Vifo vya Mama na Mtoto hafla hiyo iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Bank kupitia Kampeni ya AMREF iitwayo Stand Up for Tanzania Mother iliyozinduliwa mnamo tarehe 15 Mei 2013.

Mwenyekiti wa Benki M ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mh Nimrodi Mkono Akitoa neno kwa wageni waalikwa katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani kwaajili ya kuchangisha pesa ya kusomesha wakunga, Hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jana Usiku Huku ikiwa imeandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage na Benki M kupitia Kampeni ijulikanayo Stand Up for Tanzania Mothers

Mmoja wa Wanafunzi wa Masomo ya Ukunga Kutoka Katika Jamii ya Wafugaji kutoka Kilindi Bi Tanioi Moringe Akitoa shukrani zake za dhati Kwa AMREF Tanzania ambao ndio Wameweza kumdhamini Kumsomesha Katika Chuo Cha Ukunga.

Makamu wa Raisi Mh Dk Mohamed Gharib Bilal ambae pia alikua Mgeni rasmi katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M akipokea mfano wa Hundi yenye Thamani ya Shilingi Milioni 25 za Kitanzania kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya NBC kwaajili ya MChango wao katika Kampeni ya Stand up For Tanzania Mother ambayo inalengo la kukusanya pesa kwaajili ya Kusomesha wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto
 Mgeni Rasmi Ambaye pia Ni Makamu wa Raisi Wa Tanzania Mh Dk Mohamedi Gharib Bilal akitoa Vyeti vya kushukuru kwa wawakilishi wa Makampuni yaliyoweza kudhamini usiku huo wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M hafla iliyofanyika jana Usiku katika Hotel ya Serena
 Baadhi ya Wawakilishi wa Makampuni yaliyoweza kudhamini Hafla ya Usiku wa Chakula Cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benk M wakipokea vyeti vya Shukrani kutoka Mgeni Rasmi Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika Hotel ya Serena.
 Wadau waliohudhuria hafla ya Usiku wa Chakula Cha Hisani wakiangalia jiwe la Tanzanite lililokuwa likinadaiwa jana katika Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena



Wadau wakipata Msosi katika Hafla ya Usiku wa Chakula Cha Hisani uliofanyika jana katika Hotel ya Serena na kuandaliwa na AMREF Tanzania kwa Kushirikiana na Montage Limited na Benki M.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)