Pages

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI 22 WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAAM

photoKamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(mbele kwenye Jukwaa) akipokea Salaam ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya Uvalishaji vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo hicho tangu tarehe 19 Septemba, 2013 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Hafla hiyo imefanyikia leo Oktoba 05, 2013 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam.imageKamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha kwa sasa, Injinia Jeremiah Nkondo. Sherehe hizo za uvalishaji vyeo zimefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Serikali(hawapo pichani).image (1)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza katika hafla fupi ya Uvalishaji vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo hicho tangu  tarehe 13 Septemba, 2013. Hafla hiyo imefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
image (2)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wasaidizi Waandamizi 22 mara baada ya kuwavalisha cheo hicho leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam( wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile( wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga( wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy.
image (3)Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali vya Habari wakifanya mahojiano na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja mara baada ya hafla ya Uvalishaji Vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo hicho hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)