Pages

KAMANDA KOVA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU HALI YA UFO SARO

1 (1)KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalum jijini Dar es Salaam, Suleiman Kovaakizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hospitali ya Muhimbili.
…………………………………………………………………………………….
KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalum jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema hali ya mwandishi wa habari wa ITV Ufoo Salo aliyepigwa risasi na mchumba wake Ancel Mush, inaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Kova alisema tukio hilo linahusishwa na ugonmvi wa kifamilia ambao hadi sasa haujafahamika chanzo chake.  Kwa mujibu wa madaktari, hali ya mgonjwa ilikuwa inaendelea vizuri na alikuwa akitarajiwa kuingizwa chumba cha upasuaji nyakati za mchana jana

Akizungumzia mauaji hayo, Kova alisema japo mhusika alijiua baada ya kumuua Anastazia Salo (58), bado kitendo hicho hakiliondolei jeshi hilo haki kuchunguza kwa sababu inawezekana wapo waliyosbabisha hadi mauaji kutokea. Kova alisema wanatarajia Ufoo atakuwa miongini mwa watu watakaolisaidia jeshi hilo kupata taari zaidi za tukio la mauaji hayo.

Ofisa Mpelelezi wa Makosa ya Jinai, Ahmed Msangi alisema hasi sasa hakuna taarifa kamili bali alichoweza kusema ni kwamba jeshi limejigawa sehemu tatu ambpo kila kundi lilikuwa likikusanya taarifa.  Alisema alisema baada ya makundi hayo ambayo yalikuwa katika maeneo ya nyumbani lilikotokea tukio, Tumbi hospitali na Muhimbili, yatakusanya taarifa na kuzitoa kwa waandishi wa habari.

 Reginald Mengi, alisema kipindi hicho Madaktari walikuwa wakiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kukamilisha upasuaji “Hali yake sio mbaya inaendelea vizuri akiwa chini ya madaktari”alisema Mengi.  Alisema wanatarajia taarifa zaidi zitatolewa na msemaji wa hospitali hiyo ya Taifa Muhimbili. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)