Pages

DK. CHARLES KIMEI ,MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC

Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni Ubalozini Tanzania House,Washington DC.
Mazungumzo yakiendelea yaliyomshirikisha Dk.Kimei, Maofisa wake Waandamizi kutoka CRDB, Bw.Shumake na Mhe.Balozi Mulamula.
Dk. Kimei akimkabidhi Bw. Shumake zawadi ya kumbukumbu kutoka benki ya CRDB.
Dk.Kimei akimkabidhi Mhe.Balozi Liberata Mulamula zawadi kutoka benki hiyo.
Mhe.Balozi Mulamula akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei. Wengine kushoto ni Bw. Kenneth Kasigila,Msaidizi wa Dk. Kimei na Bw. Alex Ngusaru, Mkurugenzi wa Hazina CRDB na Bw.Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Charles Kimei jana alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambayo yalilenga katika kuimarisha huduma za benki hiyo nchini Marekani. Itakumbukwa kwamba benki ya CRDB ilikuwaa benki ya kwanza kutoka nchini Tanzania kutuma maofisa wake nchini Marekani ikiwa ni katika juhudi zake za kuwafikia wateja wenye asili ya Tanzania nchini humu. Ziara ya Bw. Kimei imekuja wakati muafaka na imezingatia katika kuboresha huduma za benki hiyo kwa wateja wake wa Marekani. Bw. Kimei alifarijika kupata taarifa mbali kutoka kwa Mhe.Balozi Mulamula ambazo zitasaidia katika kutoa huduma katika kiwango cha juu.

Kwa upande mwingine Dk. Charles Kimei alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Bw. Robert Shumake, Balozi wa Heshima wa Tanzania katika jimbo la Michigan ambayo yalihudhuriwa pia na Mhe.Balozi Liberata Mulamula. Mazungumzo baina ya Dk. Kimei na Bw. Shumake yalijikita zaidi katika kuainisha maeneo ya mashirikiano kati ya Benki ya CRDB na Kampuni ya Shumake Global Partners ya Bw. Shumake yenye makao yake Detroit,Michigan. Katika mazungumzo hayo baina Bw.Shumake na Dk.Kimei yalihudhuriwa pia na Bibi Tully M., Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, Bw.Alex Ngusaru Mkurugenzi wa Hazina (CRDB) na Bw.Kenneth Kasigila, Msaidizi wa Dk.Kimei.

Pichani Dk.Kimei katika taswira mbali mbali alipokuwa Ubalozini wa Tanzania Washington DC.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)