Pages

CRDB BANK YAFANYA HAFLA FUPI UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC NCHINI MAREKANI

Mhe. Balozi Liberata Mulaula katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei wakati wageni wakiingia kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza huduma mpya za kibenki kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiingia kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulikofanyika hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank Jumatano Oct 9, 2013 kwa ajili ya kutambulisha huduma mpya za Benki hiyo kwa ajili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatamburisha waheshimiwa wageni kwa baadhi ya Watanzania walofika kusikiliza huduma mpya za Benki ya CRDB kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite na baadae kumkaribisha mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei kuongea na WanDMV kwa niaba ya WanaDiaspora.
Mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank, Dkt Charles Kimei akielezea huduma hizo mpya ambazo ni JIJENGE (Mortgage Finance) na FAHARI HUDUMA (Argent Banking) na pia alielezea maboresho ya hudma ya Tanzanite ikiwemo mteja anapofkisha kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti yake hakutakuwa na makato ya aina yeyote yatakayokatwa kila mwezi.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiongea machache na kuwaambia wanaDMV wajisikie wapo Tanzania na salama kwani amekuja na ujumbe mzito unaowakilisha Bara na visiwani na baadae kumshukuru Mhe. Balozi Mulamula kwa makaribisho mazuri na CRDB Bank kwa kuandaa hafla hiyo fupi iliyofanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Jumatano Oct 9, 2013 jioni.
Waziri wa Fedha na Uchumi akiongoza ujumbe wake kwenye chakula cha jioni.
Duputy Governor Economic & Financial Policies Dkt. Natu El- maamry Mwamba akijiatia chakula cha jioni.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula nae akijipatia chakula cha jioni.
Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzaibar Mhe. Yussuf Mzee akibadilishana mawili matatu toka kushoto ni Mariam Mkama, Love Maganga na Tully Esther Mwambapa ambaye nia Director of Marketing, Reserch and Customer Service wa CRDB Bank.
Mkurugenzi mkuu wa TRA Harry Kitilya (kati) akibadilishana mawili matatu na Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Colonel Adolph Mutta (kushoto) na Afisa Ubalozi Dkt. Switebert Mkama.( Picha na Vijimambo Blog)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)