All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa
Pages
▼
BM HAIR & BEAUTY CLINIC YATIMIZA MIAKA 12 YA UTENDAJI WAKE, ILIANZA NA WAFANYAKAZI 3 SASA IMEAJIRI 40
Benno Chelele Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akielezea mafanikio na changamoto ambazo wamekutana nazo katika kufikia mafanikio yao katika hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake, ambapo ilianza na wafanyakazi watatu na mpaka sasa imefikisha wafanyakazi 40 huku ikiwa ni mpiango ya kupanua huduma zake zaidi kwa kuzipeleka mikoani na baadae Afrika Mashariki kwa ujumla, Kampuni hiyo pia ina mipango ya muda mrefu ya kutekeleza mradi wa jengo kubwa la ghorofa utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, Hafla hiyo imefanyika jana kwenye ofisi zao zilizoko Kinondoni kwa Manyanya jijini Dar es salaam Hizi ni baadhi ya mashine za kutolea huduma katika saluni hiyohili ni duka lililomo ndani ya saluni hiyoKeki ilikuwa hiviMkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele akitoa neno la shukurani kwa wafanyakazi na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu ambaye pia ni mke wake kushoto.Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu wakitoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo Bernald Samwel.Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu wakitoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo Diana KyaruziMkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu wakitoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo Bernald Samwel.Hassan RashidMkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu wakitoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo Regina Mahengawafanyakazi wa kampuni hiyo wakifungua chupa za mvinyo (Champagne) wakati wa hafla hiyo.Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu pamoja na wafanyakazi wakinyanua glasi za mvinyo juu kama ishara ya kusherehekea miaka 12 ya kampuni yao.Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu pamoja na baadhi ya wafanyakzi wakikata keki kusherehekea kampuni hiyo kutimiza miaka 12 ya utendaji wake.Mkurugenzi wa kampuni hiyo Benno Chelele kulia na Mkurugenzi mwenzake Magreth Makungu ambaye pia ni mke wake wakilishana keki kama ishara ya kusherehekea kampuni yao kutimiza miaka 12 ya utendaji wake katika hafla iliyofanyika ofisini kwa Kionondoni kwa Manyanya.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)