Pages

WANAJESHI 7 WALIOUAWA DARFUR FULL STORY


Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imeingia kwenye majonzi mazito baada ya wanajeshi wake 7 kuuawa na waasi wa Jimbo la Darfur nchini Sudan inayoongozwa na Rais Omary Bashir walipokuwa katika kazi ya ulinzi wa amani nchini humo.

Imam akiongoza sala ya kuaga miili ya wanajeshi waliouawa Darfur nchini Sudan.
Pamoja na tukio hilo la kusikitisha, Risasi Mchanganyiko limechimba kwa undani na kuibuka na ‘full story’ ya kilichotokea siku ya tukio na kusababisha wanajeshi hao kuuawa.
Kiongozi wa Kanisa naye akiongoza sala ya kuaga miili ya wanajeshi hao.
HABARI KAMILI
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo cha kuaminika, wanajeshi wa Tanzania walikuwa wakiusindikiza msafara wa amani wa Umoja wa Mataifa (UN) uliokuwa ukitokea eneo la Khor Abeche kwenda Nyara Darfur na kushambuliwa na waasi hao.

Msemaji wa Jeshi la Tanzania, Kapambala Mgawe.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kabla ya shambulio hilo, lililowaondoa duniani wanajeshi hao, inadaiwa kwamba mmoja wa wanajeshi wa Tanzania alitekwa na waasi hao ambao walikuwa na nia ya kutaka kumshikilia na kutoa vitisho kwa dunia kuondoa majeshi yanayolinda amani nchini humo. Inadaiwa kuwa wanajeshi wa Tanzania walihamaki na kujaribu kutoa msaada wa kumuokoa mwenzao ndipo lilipotokea shambulio hilo ambalo pia limesababisha wanajeshi wengine 14 kupatwa na majeraha.
Rais Jakaya Kikwete.
KUMBE WANGEFANYA HIVI…
Wanajeshi hao wa Tanzania wameuawa wakiwa wanapigania amani na kutii kifungu cha 6 cha sheria cha majeshi ya kulinda amani duniani ambacho kinapiga marufuku wanajeshi kujibishana kwa silaha na waasi.
Wanachotakiwa kufanya ni kukimbia au kujilinda kwa kujihami bila ya kuleta madhara kwa upande wa pili vinginevyo wasingekufa kama wasingeitii sheria hiyo.

TANZANIA YALIA NA KIFUNGU NA.6
Akizungumza na waandishi wa habari nchini mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa Jeshi la Tanzania, Kapambala Mgawe alisema Tanzania inatarajia kufanya mazungumzo na Umoja wa Mataifa (UN) ili kuomba kifungu hicho namba 6 kinachowakataza wanajeshi wanaolinda amani kujibu mapigo kiondolewe.

Rais wa Sudan Omar Hassan Ahmad Al-Bashir.
VILIO KILA KONA
Pamoja na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuwalilia wanajeshi hao, vilio vimetawala kila kona ya nchi.

HEBU ONA
Kutokana na asili ya majina ya wanajeshi hao, kila pembe ya nchi inaweza kuguswa kwa njia moja ama nyingine na vifo hivyo;
Sajenti Shaibu Othuman na Koplo Mohammed Juma, hawa wanawakilisha vilio upande wa Pwani ya Tanzania kuanzia Zanzibar hadi Kusini mwa Tanzania kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wanajeshi wakiaga miili ya wenzao.
Wengine ni Koplo Oswald Chaula na Pte. (Private) Rodney Ndunguru, hawa wanawakilisha Nyanda za Juu Kusini  katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma.
Wakati marehemu Pte. Peter Werema anawakilisha Kanda ya Ziwa hususan katika Mkoa wa Mara ambao sambamba na mikoa mingine ya jirani nao wameguswa na msiba huo.
Kilio hicho kimesambaa hadi katika mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania ikiwemo Arusha na Kilimanjaro kutokana na kifo cha Pte. Fortunatus Msofe .
Aidha, mwanajeshi mwingine Koplo Mohammed Chikilizo naye amesababisha vilio katika mikoa ya Pwani.

Miili ikipandishwa kwenye gari tayari kwa safari ya Tanzania.Habari Kwa Hisani ya Tovuti ya Global Publisher

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)