Pages

TAMASHA KUBWA LA MUZIKI NA MITINDO KUFANYIKA NCHINI KENYA MWISHONI MWA WIKI HII


Wasanii kutoka Nigeria, Panshak Zamani, anayejulikana zaidi kwa jina la Ice Prince(Pichani juu, pamoja na David Adedeji Adeleke(Pichani chini kabisa), wanatarajia kuwa wasanii wakubwa watakaoitikisa Kenya mwishoni mwa wiki hii katika tamasha kubwa la muziki na mitindo linalojulikana kwa jina la Boombataa Festival.

Wasanii pekee kutoka kernya watakaoshiriki tamasha hilo ambalo ni la kwanza kufanyika, ni Victoria Kimani, Sound Afrique Band na Sauti Sol, huku wasanii wengine wakubwa watakaoonekana katika tamasha hilo wakitajwa kuwa ni Monster Djs na Purpl Dj.

Kampuni ya Adrenaline, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo wameiambia mwananchi kwamba litakuwa tamasha la mfano kwa Afrika Mashariki nzima na linatarajia kuvuta maelfu ya watu kuhudhuria kutokana na kuleta wasanii wakubwa na wa kimataifa.

Ice Prince anayetamba na nyimbo kama Oleku, Olofofo, Superstar na Baby anatarajia kufanya onesho lake la kwanza nchini Kenya tarehe 27 ya mwezi huu ambapo ataambatana na mwanamuziki mwenzake Davido ambaye pia anajulikana kupitia wimbo wake mpya wa Gobe, uliovunja rekodi ya kuangaliwa mara milioni moja kwa dakika 25, ulipowekwa kwenye mtandao wa Youtube.

Homa ya kuwasili kwa wasanii hao imesababisha wasanii kutoka kenya kupania tamasha hilo huku dhamira ikiwa kuwafunika wanigeria hao wanaotamba katika medani ya muziki duniani kote ambapo SautiSol, wamekuwa waki’twee’ mara kwa mara kuongelea jinsi watakavyoonesha maajabu katika tamasha hilo.

Tamasha hilo kubwa na la kimataifa linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ngong Race Course

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)