Pages

SAUREZ ATACHEZA KESHO KUTWA KWA MARA YA KWANZA TANGU AMNG`ATE IVANOVIC, RODGERS ASEMA HAONDOKI ANFILED

Stuck in the middle: Luis Suarez is training with Liverpool against after arriving in Australia on SaturdayLuis Suarez akifanya mazoezi na kikosi cha majogoo wa jiji baada ya kuwasili nchini Australia jumamosi ya wiki iliyopita
Stuck in the middle: Luis Suarez is training with Liverpool against after arriving in Australia on Saturday
Stuck in the middle: Luis Suarez is training with Liverpool against after arriving in Australia on Saturday
Stuck in the middle: Luis Suarez is training with Liverpool against after arriving in Australia on Saturday
 Suarez alifanya mazoezi AMMI leo hii na kuonekana ana morali kubwa katika kibarua cheka katika klabu ya Liverpool
Meet and greet: Suarez only arrived in Melbourne on Saturday night Amefika na kuwapa hai: Suarez baada ya kuwasili Melbourne jumamosi usiku
Still got it: Fans lined the street as Suarez and his Liverpool team-mates arrived at their hotel Mashabiki walijipanga mitaani wakati Suarez na klabu yake ya Liverpool ilipokuwa inawasili hotelini
High spirits: Brendan Rodgers spoke to journalists ahead of the match against the Melbourne side Morali ya juu: Brendan Rodgers akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mechi dhidi ya Melbourne
Captain fantastic: Steven Gerrard was also with the squad ahead of the pre-season game Nahodha aliyetukuka Anfiled,  Steven Gerrard pia atakuwepo katika kikosi cha Liverpool
 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com

Mshambuliaji hatari wa Liverpool, Luis Suarez anatarajia kuichezea klabu yake kwa mara ya kwanza katika mchezo wa pili wa maandalizi ya ligi kuu soka nchini England mjini Melbournekeshokutwa  tangu afanye kitendo kibaya cha kumng`ata  beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.


Suarez aliwasili Australia jumamosi ya wiki iliyopita akitokea mapumzikoni na sasa yupo na kikosi cha  Brendan Rodgers, huku kocha huyo akisisitiza kuwa nyota wake atabakia Anfield.

Mechi hiyo ya kesho kutwa  meneja wa majogoo wa jiji anatarajia kumpanga mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ambaye hajatulia kwa sasa klabuni  kuongoza safu ya ushambulizi dhidi ya Melbourne Victory katika dimba la MCG, lakini kabla ya mechi hiyo Rodgers anatarajia kuzungumza na Suarez kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.

 Suarez ambaye amekuwa gumzo katika hekaheka za usajili, akihusishwa na mpango wa kutaka kuihama klabu yake, huku Arsenal wakiwa mstari wa mbele kuitaka saini yake kwa ada ya uhamisho ya pauni 40, lakini hali aliyoionesha wakati akiwasili Austaria inabadili mawazo ya wengi hususani baada ya kukataa kuongea na waandishi wa habari juu ya maisha yake ya msimu ujao.
 
Wakati huo huo kocha wake Rodgers alisisitiza kuwa matarajio yake ni kuwa Saurez atabakia Anfield msimu ujao na klabu yake haina mpango wa kumuuza.

Kuelekea mchezo wa kesho kutwa dhidi ya Melbourne Victory, tayari mpaka sasa tiketi 90,000 zimeshauzwa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)