Pages

LOWASSA AMSIFIA KIKWETE

Na Swahili TV
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa, amemsifia Rais  Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima  katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani  Bwana Barack Obama kuja nchini na
viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa  kumeonyesha Rais Kikwete  anakubalika.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais  Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine  labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.

Pia alisema  Rais Kikwete amekuwa akihusishwa  na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.
Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana  katika nchi moja kwa wakati mmoja,  Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.

kwa habari zaidi tembelea Swahili TV Blog 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)