Pages

JUST IN:LORI LILILOKUWA LIMEBEBA SHEHENA YA MABOMBA LASHAMBULIWA NA MAWE MJINI MTWARA NA DEREVA KUJERUHIWA VIBAYA MUDA MFUPI ULIOPITA

Habari zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva Wa lori hilo Kujeruhiwa Vibaya. Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika manispaa ya mikinda Mtwara Mjini Sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile kinacho dhihirisha kua wana Mtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka Kusafirisha Gesi hiyo kwaajili ya Manufaa ya Nchi. Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi  Mtwara, Ikiwa
ni wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar.

Source: Jamii Forum

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)