Pages

IGP Said Mwema akutana na Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam

_DSC9470Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akimkabidhi zawadi yenye nembo ya Jeshi Polisi Tanzania, Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku sita hapa nchini.

_DSC8682Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur (wapili kutoka kulia), akitoa mada katika kikao cha kubadilishana uzoefu kilichowashirikisha makamishina na maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini. Kutoka kulia ni Kamishina wa utawala na fedha wa jeshi la polisi, CP Clodwig Mtweve, Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Paul Chagonja, Mkuu wa tathmini na ufuatiliaji Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Omar Rashid pamoja na Mkuu wa Utawala na rasilimali wa jeshi la Polisi (DCP)Thobias Andengenye.( Picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)