Pages

BASI LA NAJMUNISA LAPASUKA GURUDUMU KISHA KUPINDUKA NA KUUA MUDA MFUPI ULIOPITA


                     Kamanda David Misime.

Watu wanne waliokuwa wanasafiri kwa basi la kampuni ya Najmunisa wamekufa papo hapo baada ya basi hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kupata ajali eneo la Mbande, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi lilipinduka baada ya tairi la mbele kupasuka na kugonga mti, huku wanne hao wakifa papo hapo na wengine wakijeruhiwa vibaya, kiasi cha kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime amethibitisha kutokea kwa ajali
: SOURCE ziro99 blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)