Pages

Shukrani Kutoka Kwa Familia ya Herbert Johnson Mwaimu


Familia ya Herbert Johnson Mwaimu, inatoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao Charles Alan Hiza Herbert Mwaimu kwenye misa iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Albano Dar-es-Salaam. 

Pia katika misa iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Raphael Mdote  Michungwani , Muheza Tanga na hatimae maziko yake kijijini Kwegoe Muheza Tanga.

Shukrani zwaendee ndugu, jamaa na marafiki ambao walikuwepo kuwafariji na hata kupiga simu za kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu, madaktari na wauguzi wa hospitali za Tanzania Heart Institute na Agha Khan za Dar-es-Salaam na hospitali ya Peramiho ya Songea.

Shukrani za pekee ziwaendee bwana Sebastian na bwana Khalid.

Shukrani za pekee ziwaendee mapadre na maaskofu wa Anglikana kwa kusimamia kufanikisha misa ya wafu kwenye kanisa la Mtakatifu Albano Dar-es-Salaam.

Shukrani za pekee kwa padre wa kanisa la mtakatifu Raphael Mdote Michungwani Muheza Tanga. Shukrani za pekee ziwandee wanafamilia wa Katumba, familia ya Mwakijambile na familia ya kaka Tony Mapunda wa Kimara Dar-es-Salaam.

Shukrani za pekee ziwaendee madaktari Dr Masau wa Tanzania Heart Institute, Dr Mustapha, Dr Salim na Dr Mohamed wa Hospitali ya Agha Khan Dar-es-Salaam. Shukrani za pekee zimfikie mzee wetu Ahmed Suleiman Makota na familia yake. Na pia shukrani za pekee ziende kwa wajomba wa marehemu Charles na mama zake wote.

Mwisho tunatoa shukrani za pekee kwa uongozi wa NMB tawi la Mlimani City kwa msaada wao mkubwa wa hali na mali na kuhakikisha kwamba mfanyakazi mwenzao anapelekwa kijijini kwao kulala malalo ya milele.

Roho ya marehemu Charles Alan Hiza Herbert Mwaimu ipumzike kwa amani katika uzima wa milele mahala pema peponi.

Amina.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)