Pages

RAIS KIKWETE AKUTANA NA SEKRETARIETI MPYA YA CCM DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti  mpya wa CCM Bara, Philip Japhet Mangula (kulia) ikulu ndogo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wapili kushoto) akizungumza na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Sefu Iddi,Makamu mpya wa CCM Bara Bwana Philip Mangula(watatu kushoto) pamoja na makamu wa CCM Bara aliyemaliza muda wake Bwana Pius Msekwa.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo pamoja na Makamu mweyekiti mpya wa CCM Bara, Philip Mangula (Katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti Bara aliyemaliza muda wake Bwana Pius Msekwa ikulu ndogo mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Katibu Mkuu wa CCM aliyemaliza muda wake Dk.Wilson Mukama ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi. Dk.Mukama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi  cha CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete akiwa na Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Mwigulu Nchemba ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.
Mwenyekiti wa CCM Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu mpya wa oganaizesheni  ya CCM Bwana Mohamed Seif Khatib mjini Dodoma.Picha zote na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)