Pages

MWANDISHI WA HABARI WA SIBUKA LULU OSCAR AFARIKI DUNIA JANA

Mwandishi wa Sibuka afariki dunia kuzikwa Alhamisi
 
NA Andrew Chale
MWANDISHI wa Habari  wa kituo cha SIBUKA, aliekuwa akitangaza na kuandaa vipindi mbalimbali kikiwemo cha Pepeta Afrika, Lulu Oscar amefariki dunia jana Jumanne  nyumbani kwao Mbezi Kwa Yusufu.
 
Akizungumza na .. mtandao/gazeti  mdogo wa marehemu, Ritha Oscar alisema kuwa  Lulu alipatwa na mauti hayo majira ya usiku ambapo alizidiwa ghafla kufuatia kulalamikia kifua kumbana.
 
“Awali alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Masister  ya Luguluni kule Mbezi, zaidi ya mara tatu,  jana aliruhusiw kurudi nyumbani lakini baada ya kuendelea vizuri lakini jioni usuku alilalamikia kifua kikimbana  tulimuangaikia mpaka hatua ya mwisho lakini ikashindikana na alipoteza maisha” alisema Ritha kwa masikitiko makubwa.
 
Ritha alisema kuondoka kwa Lulu kwenye familia yao ni pigo kubwa kwani alikuwa bado ni mdogo na alikuwa msaada mkubwa kwa ndugu na jamaa.
 
Aidha, alisema kuwa, kikao cha muda cha ndugu kilichokaa wameafikiana kuzikwa siku ya Alhamisi katika Makaburio ya Kinondoni. “Mpaka sasa taarifa za familia, ni kuwa mazishi yatakuwa siku ya Alhamisi pale mkaburi ya Kinondoni na msafara utaanzia nyumbani Mbezi kwa Yusufu na kuelekea Makaburini” alisema Ritha.
 
Marehemu alikuwa mwajiliwa wa televisheni ya SIBUKA (TV SIBUKA) akiwa kama mtangazaji na mwandaaji wa vipindi ambapo pia alikuwa akiandaa na kutangaza kipindi cha Pepeta Afrika, kilichojizola umaarufu mkubwa mpaka anakufa kwake.
 
Katika historia yake, Lulu  alihitimu elimu yake  ya msingi alihitimu mwaka 1996 katika shule ya Upanga na kwa elimu ya uandishi wa habari alisomea chuo cha Royal College of Tanzania  na baadae mwaka 2003, aliweza kuhitimu kozi zake hiyo ya juu katiika Taasisi ya uandishi wa habari na mawasiliano Institute of journalisim and mass communication.
Marehemu alikuwa hajaolewa wala hajaacha mtoto.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)