Pages

MKAKATI WA UTANGAZAJI UTALII KUZINDULIWA 15/11/2012.

Na: Geofrey Tengeneza

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki anatarajiwa kuzindua mkakati wa utangazaji utalii wa kimataifa tarehe 15/11/2012 katika hoteli ya Serena hapa jijini Dar es salaam.

Mkakati huo unaotarajiwa kuwa ndio dira ya kuitangaza Tanzania kama eneo la utalii duniani  umetengenezwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) linajumuisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii hapa nchini.

Hafla hiyo itakayofanyika kuanzia saa 12.30 jioni itahudhuriwa pia na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi, Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Milao na viongozi wengine  kutoka Wizarani. Aidha viongozi wa Shirikisho la vyama vya utalii nchini TCT na wadau wengine wa sekta ya utalii watahudhuria pia hafla hiyo.

1 comment:

  1. Anonymous9:18 AM

    Fine!! Lakini vipi kuhusu utalii wa ndani? Kuna hatua zipi zinatekelezwa kwa ajili ya utalii wa ndani?
    Kwanini kila wizara,au sekta,au shirika la kibinafsi au la kiserikali lisitenge wiki moja katika mwaka,iitwe "WIKI YA UTALII" ili wafanyakazi na watumishi wapate fursa hiyo?? LET US REASONING ABOUT THIS TOGETHER!!

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)