Fastjet, Shirika la ndege la
kwanza Afrika linalotoza nauli nafuu, leo limezindua mauzo ya tiketi
zake nchini Tanzania, ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya kwanza ya
kibiashara mwishoni mwa mwezi huu.
Uzinduzi huo wa tiketi ni hatua
muhimu katika juhudi za kampuni kuwezesha usafiri wa ndege kwa
Watanzania walio wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari
za ndege. Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32, 000 (U$D20) kabla
ya kodi za serikali, usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za
watu kusafiri.
fastjet, ambayo imeinunua Fly540,
imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza cha uendeshaji
barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa kuanza kuruka
kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia Novemba
29. Tiketi za Dar es Salaam – Kilimanjaro na Dar es Salaam – Mwanza
zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari zingine, za ndani na kanda ya
Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya wiki kadhaa.
Akizungumzia uzinduzi wa mauzo ya tiketi, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters alisema:
“Hiki ni kipindi cha kihistoria
kwa safari za anga Tanzania, na hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena
himaya ya watu wachache Tanzania. fasyjet itafanya usafiri wa anga kuwa
kitu ambacho Watanzania wengi wanakimudu tofauti na awali, na hivyo
kutoa fursa nzuri zaidi kwa biashara, safari za likizo, na wanafamilia
kutembeleana. Tunawashukuru wabia wetu Tanzania kwa ushirikiano wao
mpaka leo hii, na tunamatumaini ya uhusiano mrefu na wenye manufaa kwa
watanzania.”
Tiketi zinapatikana kupitia
mawakala wa usafiri na dawati la mauzo, kituo cha mawasiliano na ofisi
za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet, www.fastjet,com itazinduliwa
wiki ijayo na kutoa taarifa za safari na nauli. Tovuti hiyo pia
itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za credit/debit pamoja na simu
za mkononi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)