Meneja
Mwendeshaji wa Kampuni ya Joker Club Olec Aleksejev kulia akitunishiana
misuri na bondia wa timu ya Taifa ya Masumbwi Said Hofu baada ya
kumkabizi vifaa kwa ajili ya mchezo huo baasda ya kuibuka mcherzaji bora
wa mashindano kati ya Zambia na Tanzania
|
Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) akizuia ngumi nzito za Mbachi Kaonga wa Zambia kg 75 |
MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita wamechezea kichapo baada ya
kupigwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa na mabondia toka
Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo
Mapambano haya ambayo yalikuwa ni ya kirafiki ya kimataifa
yanayojulikana na Shirikisho la ngumi za Ridhaa Duniani AIBA yenye
raundi tatu
ilishuhudia Said Hofu akifungua pazia (kg 49) kwa kupigwa kwa pointi na
Caristo Bwalia toka Zambia
Mpambano wa pili kg 56 ulishuhudia Frank Nicolaus wa Tanzania akipigwa na Russel Mwamba wa Zambia kwa pointi pia.
Kg 60 ndipo mtanzania Ismail Galiatano alimshushia ngumi nzito nzito
John Chimpwele wa Zambia na kusababisha kuchanika juu ya jicho na
kutokwa damu nyingi ndipo mwamuzi alisimamisha mchezo na kumpa ushindi
Ismail Galiatano.(RSC)
Mpambano wa nne kg 64 Mtanzania Kassim Hussein alipokea kipigo toka kwa Charles Lumbwe kwa kupigwa kwa pointi.
Funga kazi kg 75 ikawa ndio usiseme maana Mohamed Chimbumbui alipigwa
kwa TKO na Mbachi Kaonga wa Zambia baada ya kumsukumizia makonde mazito
mazito na kushindwa kuyahimili na kujikuta akianguka kila mara.
Katibu wa Chama ngumi za ridhaa, Makore Mashaga alisema wamepoteza
mpambano huo lakini anashukuru wamepata mazoezi ya kujiandaa na
mashindano ya ndano yanayotarajiwa kuanza Novemba 26 kwenye uwanja wa
ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.
Mabondia watanzania walisema kupigwa kwao kunatokana na maandalizi
hafifu waliyopata na mashindano kuahirishwa mara kwa mara pia
kuliwafanya morali kushuka.
Naye Katibu wa Ngumi za Ridhaa wa Zambia Lut. Kanali Man Muchimba
amesema amefurahi kucheza na watanzania kwani wamepata mazoezi ya
kuwasaidia kucheza mashindano ya kanda ya tano yatakayofanyika nchini
kwao mapema Desemba.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)