Pages

JENERALI WAITARA KUONGOZA WAPANDA MLIMA KILIMANJARO.

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali, George Waitara (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya maandalizi ya upandaji mlima Kilimanjaro unaotaraji kufanyika Desemba 6, 2012. Jenerali Waitara ndiye atakae ongoza upandaji huo wa mlima Kilimanjaro.Miongoni mwa taasisi na makampuni ya liyodhamini upandaji huo wa mlima Kilimanjaro ni Kampuni ya Bia ya Serengeti, Precision Air, JWTZ, Jeshi la Magereza , KJ Traders and General Supplies Ltd na Kibosho resort.
 
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali, George Waitara (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya maandalizi ya upandaji mlima Kilimanjaro unaotaraji kufanyika Desemba 6, 2012. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Balozi Charles Sanga na Mratibu wa Upandaji wa Mlima Kilimanjaro, Joseph Kitani. Jenerali Waitara ndiye atakae ongoza upandaji huo wa mlima Kilimanjaro.
 *******
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUPANDA MLIMA KILIMANJARO TAREHE 06 DESEMBA 2012, IJULIKANAYO KAMA “ANNUAL KILIMANJARO CLIMB”
Kampuni ya KJ Traders ikishirikiana na Tanzania Tourist Board (TTB) imeandaa Uhuru expedition ambayo ni mwendelezo wa kumbukumbu ya kutangaza Mlima Kilimanjaro kwa kuwashirikisha watu mbalimbali wakiongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.
 
Utaratibu wa expedition hiyo ulianza mwaka 2008 wakati huo ukiratibiwa na M/S KJ Traders na Kibosho Resort, lakini kwa sasa baadhi ya taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma nao wameingia na kuleta msisimko mpya kwa nia kukuza utalii kwa kutumia Mlima Kilimanjaro.
 
Expedition hiyo ya kupanda Mlima inatarajiwa kuanza tarehe 06 Desemba 2012 na kuhitimishwa tarehe 10 Desemba 12, na Waziri wa Maliasili na Utalii atahitimisha rasmi tukio hilo.
 
Makampuni na Taasisi za Umma ambazo zinatarajia kwa udhamini na ushirika katika tukio hilo ni
o Tanzania Tourist Board (TTB)
o Jeshi la Wanachi wa Tanzania
o Serengeti Breweries Ltd
o Jeshi la Magereza
o NMB
o KJ Traders and General Supplies Ltd
o Kibosho Resourt
 
Watu wanaotarjiwa kupanda Mlima safari hii ni Wabunge, baadhi ya wanajeshi na wananchi wa kawaida. Vilevile tunarajiwa kupata Mgeni kutoka nje ya nchi mwanachi wa Tibeti (China).
 
Kauli mbiu yetu mwaka huu ni “KUKUZA UTALII NA KUTUNZA MAZINGIRA KWA ULINZI SHIRIKISHI”. 
 
Wote mnakaribishwa.
Jenerali Mstaafu George Waitara

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)