Coca Cola Kwanza unveils Schweppes +C in Tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Coca Cola Kwanza unveils Schweppes +C in Tanzania

Mkuu wa idara ya Fedha wa Coca Cola Kwanza Bw. Erastus Mtui akifanya Interview na waandishi kwenye Uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha  Schweppes +C cha kampuni ya Coca Cola Kwanza
Mkurugenzi wa fedha (finance director) wa Coca Cola Kwanza Finance Director Mr. Erastus Mtui (wa kwanza kushoto) akiwa na Maneja Masoko na mauzo wa kampuni  ya Coca Cola Kwanza Bi. Josephine Msalilwa, Pankaj Singh Mkurugenzi wa logistics pamoja na Haji Ally Public Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wakwakiwa kwenye Uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha  Schweppes +C

Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, imezindua kinywaji kipya chenye ladha ya limao kinayojulikana kama Schweppes +C, ikiwa ni sehemu ya kuongeza machuguo ya bidhaa kwa wateja wake
Kinywaji cha Schweppes +C kinawalenga zaidi wateja wenye umri mkubwa.


Akiongea wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola ,Basil Gadzios, alisema kampuni yake imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ugunduzi na kuongeza idadi ya bidhaa tofauti tofauti ikiwa na lenga la kukidhi mahitaji ya wateja tofauti tofauti katika soko la Tanzania.


Tunayofuraha kuongeza bidhaa nyingine mpya sokoni ikiwa ni shehemu ya jitihada za kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Schweppes +C yenye ladha ya limao inawaletea wateja wetu ladha ya kipekee ya limao ikiwa na Vitamini C ambayo tunaamini wataifurahia. Kinywaji kimetengenezwa mahsusi kumpa mtumiaji wake ladha nzuri ya juisi ya limao. Tukiwa kama kampuni ya vinywaji baridi, tumejidhatiti kuwaletea wateja wetu kilicho bora na bado tuna vingi kwa ajili yao, alisema mkurugenzi huyo.


Gadzios aliongeza kuwa, Coca-Cola inatarajia kuingiza sokoni bidhaa nyingine nyingi ambazo siyo tu zitakidhi mahitaji ya jamii ya leo bali pia zitaendana na wateja ambao mahitaji yao hubadilika katika soko la kileo huku akiongeza kuwa kinywaji hicho kipya kimetengenezwa kwa kuzingaatia viwaango vyaa kimataifa kikiwa na ladha ya kipekee ya limao.


“Kuwashirikisha wateja wetu, ni moja kati ya vipao mbele vya kampuni ya Coca-Cola. Hii inatusaidia kuyafahamu mahitaji yao ambayo hubadilikakulingana na muda na hivyo kutuwezesha kuwatengenezea bidhaa zinazoendana na mahitaji na matakwa yao kuwashirikisha.



Kuongezwa kwa Vitamin C kwenye kinywaji kipya cha Schweppes +C, kunakifanya kinywaji hiki kitofautiane na vinywaji vyetu vingine vilivyopo sokoni huku kikiwapa wateja ladha murua ya limao, alieleza
Kinywaji cha Schweppes +C kitauzwa kwa shilingi 1000 kwa bei ya reja reja bei ambayo itawawezesha wateja kuweza kukifurahia

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages