BENKI YA NMB KUINUA VIJANA KUPITIA MICHEZO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

BENKI YA NMB KUINUA VIJANA KUPITIA MICHEZO

DSC_1131
Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya jezi zilizotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.

DSC_1155
Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mabegi yaliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.

DSC_1137
Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mipira iliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.

DSC_1079
Baadhi ya wachezaji wa  timu za mpira wa kikapu za Savio  na Lioness za Don Bosco Upanga wakiwa katika tukio hilo.




DSC_1164
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa (kushoto) akikabidhi sehemu ya vifaa vya michezo kwa mchezo wa mpira wa kikapu kwa wachezaji wa  timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama ufadhili wa timu hizo. Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu hizo ikiwa ni ufadhili wa timu hizo. Anaye shuhudia ni Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ngingite (wa pili kushoto) waliotoa vifaa hivyo.


BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vitabu na udhamini wa jezi, mabegi ya michezo na mipira kwa kituo cha vijana cha Don Bosco Upanga cha jijini Dar es Salaam kinachomiliki timu mbili za mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo.

Msaada huo na udhamini wa vifaa hivyo kwa kituo hicho kinachosaidia vijana umegharimu kiasi cha shilingi milioni 15, ambapo akikabidhi Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite alisema benki hiyo itaendelea kuchangia katika shughuli za kusaidia jamii pamoja na kuinua michezo nchini.

Akifafaanua katika ufadhili huo, Bw. Ngingite alisema ufadhili huo umejumuisha vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na timu ya mpira wa kikapu wanaume ya Savio na timu ya mpira wa kikapu wanawake ya Lioness zote zikilelewa na kituo hicho. 

Alisema NMB imetenga takribani shilingi bilioni moja ikiwa ni maalum kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo sekta za afya, elimu na majanga endapo yanaikumba jamii. Alisema michezo mbali na kuwa ajira kwa vijana pia inawajenga kiafya na kuwawezesha kufanya vizuri hata kwenye elimu.

Timu za mpira wa kikapu za Savio na Lioness ambazo zipo chini ya kituo cha Don Bosco Ukonga ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo, na kwa udhamini wa NMB wao wamenufaika kupata jezi za kisasa, mipira ya mchezo huo pamoja na mabegi maalum ya michezo kujiandaa na mashindano aanuai.

Kwa upande wake Mlezi wa Kituo cha Don Bosco Upanga, Padre Michael Muia aliishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili na msaada walioutoa kwa kituo hicho na kuahidi wataitumia vizuri iwe chachu ya mafanikio zaidi kwa vijana.


DSC_1120
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa (kulia) akizungumza kuishukuru NMB kwa ufadhili huo. Kulia ni Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite.
DSC_1077
Baadhi ya maofisa kutoka Benki ya NMB na vijana wa Kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano.
DSC_1104
Mlezi wa Kituo cha Don Bosco Upanga, Padre Michael Muia akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili na msaada walioutoa kwa kituo cha Vijana Don Bosco Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages