Dk Salim atoa neno juu ya mgogoro wa Palestina na Israel - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Dk Salim atoa neno juu ya mgogoro wa Palestina na Israel

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza na Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina katika mgogoro wao na taifa la Israel ilipomtembelea ofisini kwake. Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza na Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina katika mgogoro wao na taifa la Israel ilipomtembelea ofisini kwake. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo. Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina wakiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim. Sehemu ya wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina wakiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina wakimkabidhi Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) kitabu cha picha za historia ya Waparestina na mgogoro huo. Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto) katika picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina mara baada ya mazungumzo. Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina wakimkabidhi Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) kitabu cha picha za historia ya Waparestina na mgogoro huo

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim amefanya mazungumzo na Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina katika mgogoro wao na taifa la Israel.

Dk Salim aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), katika mazungumzo yake na wajumbe hao amesisitiza umuhimu wa kufikiwa suluhu kwa mgogoro huo ili watu wa Palestina wapate haki zao za msingi.

Alisema kuna kila sababu ya pande zote kuheshimu maadhimio ya UN katika kufikia suluhu juu ya mgogoro huo, akizungumzia wazo la Israel kuufanya Jerusalem kuwa mji mkuu wake, alisema hali ni ngumu kwa Waparestina na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepitisha maadhimio mengu juu ya mgogoro huo lakini yamekuwa yakipuuzwa na Serikali ya Israel hivyo kuishauri kuyazingatia.

Aliipongeza Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina kwa juhudi zake za kutafuta suluhu ya mgogoro huo na kuitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kamati hiyo ili ifikie malengo yake.

Tayari viongozi wa Wapalestina wamelaani hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na kusema hatua hiyo ni kufifisha juhudi za kutafuta amani Mashariki ya Kati.

Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina mara baada ya mazungumzo na Dk. Salim Ahmed Salim walimkabidhi kitabu cha picha za historia ya Waparestina na mgogoro huo.

Hata hivyo, Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotetea haki za msingi za Wapalestina inatarajiwa kukutana na kujadiliana juu ya hatua ya Israel kutaka kuutangaza mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages