TAASISI YA DORIS MOLLEL YAZINDUA FILAMU YA MTOTO "NJITI" JIJINI DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAZINDUA FILAMU YA MTOTO "NJITI" JIJINI DAR

Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", Waziri wa Madini, Angella Kairuki (katikati) akiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kulia) pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF) na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", Doris Mollel baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa sinema wa Cinemax, Dar Free Market, jijini Dar es salaam leo. Filamu hiyo ambayo inaelezea maisha ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati "Njiti" imeandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel, imelenga kutoa elimu ya uelewa wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati.
Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", Waziri wa Madini, Angella Kairuki akitoa hotuba yake, ambapo alitoa pongezi nyingi kwa Taasisi ya Doris Mollel kwa kufanikisha kupatikana kwa elimu ya uelewa wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati kupitia filamu hiyo.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa filamu fupi ya "Njiti", ambayo inaelezea maisha ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati "Njiti"
iliyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel, imelenga kutoa elimu ya uelewa
wa namna ya malezi bora kwa mtoto anayezaliwa kabla ya wakati.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF) na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", Doris Mollel akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa sinema wa Cinemax, Dar Free Market, jijini Dar es salaam leo. 
Sehemu ya wageni waliohudhulia hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages