Polisi azua taflani mkutano wa Chadema, na kunusurika kipigo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Polisi azua taflani mkutano wa Chadema, na kunusurika kipigo

Na Bryceson Mathias, Kikombo
ASKARI Polisi wa Kata ya Kikombo  aliyejulikana kwa jina Moja la Sivanus (pichani), Jana alizua Tafrani kwenye Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya Kumnyanganya Kipaza Sauti (Mike) Katibu wa Wilaya wa Dodoma Mjini, Jella Mambo.
Silvanus alizua hayo Julai 26, ambapo alinusurika Kipigo cha Wananchi  waliokuwa na hasira kwa kufanya tukio hilo, ambapo walidai hata kungekuwa na makosa ya Matamko au kitu kingine chaochote, hakustahili kuingia jukwani na kumnyang’anya Kipaza sauti Katibu huyo.
Askari Silvanus aliyeonekana kulewa na kuwaacha wenzie kwenye gari, alichukuwa hatua hiyo, Mambo alipomtambulisha aliyekuwa Mgombea wa Chadema Kata hiyo, Yona Kusaja, kwamba, uchaguzi uliopita Kusaja hakushindwa ila Chama Tawala (CCM) kilichakachua kura zake na kutoa vitisho kwa wapiga kura.
“Upinzani Dodoma uliasisiwa na Kusaja aliposhinda kuwa Diwani na alitoa Changamoto kwenye Vikao vya Halmashauri nikiwa CCM, na walipotaka kunipiga chini kwa hila nisiwatetee wananchi wa Makulu, Kusaja aliniongoza kuchukua Fomu za Chadema, nikashinda”.alisema Ally Biringi.
Katibu wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) la Wilaya ya Dodoma Mjini, Margreth Thedai alisema, Kama si Busara ya Diwani wa Dodoma Makulu, Biringi, kumsihi arudishe kipaza sauti hicho, Wananchi wasingemvumilia wangempa Kichapo kitakatifu, maana ndiye alianza vurugu.
Mbali ya Wananchi kuahidi kumrudisha Kusaja kutokana nakile walichowaunga mkono viongozi wa Chadema kuwa wamepigika alisema, “Kwa miaka Miwili CCM katika Kata imeshindwa kuezeka Madarasa ya Shule ya Msingi yaliyoezuliwa, kutokana na fedha kulambwa na Viongozi”.
Aidha licha ya kumshangilia Kusaja, Wananchi walidai Mkutanoni kwamba, Hawamtaki Mtendaji wa Kijiji, Mwenyekiti na Halmashauri kutokkana na kushindwa kusoma mapato na matumizi ya kila mwaka, wakihofia kua za Minara, ambazo zimelambwa kisirisiri.
Kwa upande wao wananchi walidai, Polisi Silvanus alitumika kama Chambo ili awachokoze wampige, iwe sababu ya kupiga mobomu kuvuruga Mkutano wa Chadema, kwa sababu awali CCM walitakaa kufanya Mkutano wakakosa watu na kuahirisha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages