JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA SIKU YA SABA SABA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA SIKU YA SABA SABA




















Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond  pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa

Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni  Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na  Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D'  watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages